JENGA KWA UHAKIKA,JENGA NA GULYA!
Kuhusu Gulya Group Limited
Gulya Group Limited ni kampuni ya Kitanzania iliyobobea katika uuzaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi kwa wateja wa aina zote – kuanzia mafundi wa kawaida, wakandarasi wakubwa hadi watu binafsi wanaojenga nyumba au miradi ya maendeleo.
Tukiwa na makao makuu katika jiji la Dar es Salaam, tunajivunia kuhudumia wateja kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia bidhaa bora kama saruji(cement), misumari, bati, mabomba, vigae(tiles), rangi za kupaka ukutani.
Tunafanya kazi kwa karibu na wazalishaji na wasambazaji wakubwa ili kuhakikisha bidhaa tunazouza ni imara, salama, na zenye viwango vya kimataifa.
Gulya Group Limited inasimamia maadili ya uaminifu, ubora wa huduma, uwazi na kuheshimu wateja wake. Tunaamini katika kujenga mahusiano ya kudumu na wateja wetu kwa kuwahakikishia huduma ya kitaalamu, haraka, na yenye kujali thamani ya pesa yao.
Kwa mtazamo chanya na maono makubwa, Gulya Group Limited inaendelea kupanua huduma zake na kushirikiana na taasisi mbalimbali katika sekta ya ujenzi, ikiwa na lengo la kuwa moja ya kampuni zinazoongoza katika usambazaji wa vifaa vya ujenzi ndani na nje ya Tanzania.






Historia ya Kampuni
Gulya Group Limited ilianzishwa rasmi mwaka 2022 na mwanzilishi wake Bwana,Michael Alsen Bujiku, ikiwa na lengo kuu la kutoa vifaa bora vya ujenzi kwa wananchi wa Tanzania kwa bei nafuu na huduma ya kuaminika. Kampuni ilianza kama biashara ndogo ya familia lakini kwa bidii na maono ya mbali, ikakua hadi kuwa moja ya wasambazaji wanaoaminika wa vifaa vya ujenzi katika mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.
Tangu kuanzishwa kwake, Gulya Group Limited imejipambanua kwa kutoa bidhaa bora kama saruji, nondo, bati, rangi, misumari, mchanga, kokoto na vifaa vingine muhimu vya ujenzi. Tunajivunia kushirikiana na wakandarasi, mafundi, na wateja binafsi katika kuhakikisha kuwa miradi yao inakamilika kwa ubora unaotakiwa.
Tukiwa tunazingatia maadili ya uaminifu, ubora na huduma bora kwa wateja, Gulya Group Limited inaendelea kukua na kupanua huduma zake ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Miradi Yetu
Tunaweza kusaidia katika miradi yako ya ujenzi kwa vifaa bora.


Huduma zetu
Tunatoa vifaa vya ujenzi kwa wateja binafsi na wakandarasi wakubwa, kuhakikisha ubora na huduma bora katika kila mradi tunaoendesha nchini Tanzania.
Ufanisi wetu
Tumejijengea sifa nzuri katika sekta ya ujenzi kwa kutoa bidhaa bora na huduma za kipekee, tukihudumia wateja wetu kwa uaminifu na kujitolea.
Maoni Wateja
Wateja wetu wanaridhika na huduma zetu bora na bidhaa zetu.
Nimefurahia sana huduma ya Gulya Group Limited, bidhaa zao ni za ubora wa juu na zinapatikana kwa bei nafuu. Nitawapigia tena.
Amani M.
Dar es Salaam
Huduma ya Gulya Group ni bora sana. Nimepata vifaa vyote nilivyohitaji kwa urahisi na haraka. Ninawashauri wote wajaribu.
Juma K.
Dodoma